maping at Mkunguge
ߊ߬ ߟߊߦߟߍ߬ߣߍ߲߬ ߦߋ߫ Annaviola Lema ߓߟߏ߫ 23 August 2011 ߦߋ߫ Swahili (Kiswahili) ߟߋ߬ ߘߐ߫Nafurahia sana zoezi zima la kutengeneza ramani ya tandale kwan nmejifunza teknolojia mpya katika kuwakilisha hali halisi kati makazi,namna watu wanavyoishi,matatizo yanayowakabili na ni matukio gana yanakuwa yakitoea siku hadi siku katika jamii inayowazunguka watu,changamoto kubwa ni jinsi gani tunaweza kutatua matatizo hayo bila kuharibu utaratibu mzima wa maisha ya watu wa tandale na kazi zao za kiuchumi.
kubwa nililiona watanzania hatuna tabia ya kutunza mazingira yetu katika hali ya usafi haiwezekan mtu analalamika kuwa hakuna miundo mbinu kama mifereji ya maji machafu na iliyopo inatumika kama sehemu ya kutupa uchafu tena wa taka ngumu ,kuna utaratibu umewekwa na halimashauri gari la uchafu linapita kila wiki bado watu wanaendelea kutupa uchafu kila mahali.
Tunalalamika serikali yetu haitusaidii kitu chochote je kutupa uchafu holela ni swala linalohitaji serikal....na hakuna asiyejua kuwa uchafu ni hatari kwa afya na mazingira ya binadam.