RAMANI KATIKA MAKAZI HOLELA ZINAONEKANAJE?
Δημοσιεύτηκε από τον/την REGINALD στις 10 Οκτώβριος 2011 στα Swahili (Kiswahili).Kwa Tanzania bado sana suala la ramani halionekani kuwa muhimu hasa kwa wanajamii wa jamii duni kama Tandale, Manzese, (baadhi tu ya viyunga vya jiji la Dar es salaam ambovyo wanaishi watu duni). ila kama elimu ya ramani itazidi kutolewa na umuhimu wake kuonekana katika utoaji wa huduma basi itasaidiwa kujenga kujitambua kwa wanajamii hasa wa mijini kuliko na uhaba wa huduma muhimu kama maji na kusambaa kwa taka ngumu na laini kama ilivyo manzese, Tandale, Tabata na kwingine kwingi katika hili jiji la Dar es salaam